Habari za Mastaa

Kanye West amkalisha Jay Z na Drake kwa kuwa Rapper anayeingiza hela nyingi 2019

on

Forbes imemtaja rapper Kanye West kuwa ndiye anayeingiza hela nyingi zaidi duniani na kuwa rapper anayeshikilia nafasi ya kwanza ya wana HipHop wanaolipwa mkwanja mrefu zaidi 2019 ikiwa hii ndio mara yake ya kwanza, Kanye West ameingiza zaidi ya Tsh. Billioni 350 ($ 150M) kuanzia Juni 2018 hadi Juni 2019.

Taarifa zinaeleza kuwa mapato makubwa ya Kanye yametokana na mauzo ya kampuni yake ya mavazi ya ‘Yeezy” ambayo hadi mwishoni mwa mwaka huu inatarajiwa kuwa imeingiza dola Billion 1.5, huku Jay Z ambaye ndiye alikuwa akishikilia nafasi hiyo ya kwanza sasa ameshika namba mbili akiwa ameingiza zaidi ya Tsh. Billion 186 ($ 81M) na msanii Drake ambaye kwa sasa anayesikilizwa zaidi ameshika namba tatu akiwa ameingiza zaidi ya Tsh. Billioni 172 ($ 75 M)

Kwa ujumla wa mapato ya Top 20 ya rappers wote wameingiza zaidi ya Tsh. Trillioni 1.9 ($ 860) ikiwa ni 33% zaidi ya jumla ya mapato ya mwaka jana huku Rapper wa mwisho kabisa ambaye kashikilia nafasi ya 20 akiwa na Tsh. Billioni 41 ($ 18M).

Hii ndiyo list ya Top 20 rappers wanaolipwa mkwanja mrefu zaidi 2019
1. Kanye West ($150 million)
2. Jay-Z ($81 million)
3. Drake ($75 million)
4. Diddy ($70 million)
5. Travis Scott ($58 million)
6. Eminem ($50 million)
7. DJ Khaled ($40 million)
8. Kendrick Lamar ($38.5 million)
9. Migos ($36 million)
10. Childish Gambino ($35 million)
11. J. Cole ($31 million)
12. Nicki Minaj ($29 million)
13. Cardi B ($28 million)
14. Swizz Beatz ($23 million)
15. Meek Mill ($21 million)
16. Birdman ($20 million)
17. Future ($19.5 million)
18. Nas ($19 million)
19. Wiz Khalifa ($18.5 million)
20. Pitbull ($18 million)

VIDEO: MASTER JAY BAADA YA KUPEWA UJAJI MSIMU MPYA WA BSS KAFUNGUKA HAYA

Soma na hizi

Tupia Comments