Swali kubwa bado ni lini, kama Xabi Alonso ataifundisha Real Madrid, kulingana na Mkurugenzi Mtendaji wa Bayer Leverkusen Fernando Caro.
Alonso ameiongoza Leverkusen kutwaa taji lao la kwanza kabisa la Bundesliga msimu huu, na bado wanaweza kushinda DFB-Pokal na Ligi ya Europa katika msimu wa kwanza kamili wa Mhispania huyo kama meneja.
Kiungo huyo wa zamani wa Liverpool, Real Madrid na Bayern Munich alikuwa akihusishwa na kazi katika vilabu vyote vitatu msimu huu wa joto, lakini amethibitisha kuwa atasalia kuinoa Werkself msimu ujao.
Bado, akizungumza na El Larguero jana usiku, Carro alisema: “Sina shaka ataifundisha Real Madrid wakati fulani. Hakuna… Kitu pekee ambacho sina uhakika nacho ni lini. Lakini ataishia kufundisha. Real Madrid hakika.”