Breaking News

BREAKING: 15 wakamatwa DSM, ni wale wa ‘Ile pesa nitumie kwa namba hii’

on

Polisi Kanda Maalum ya DSM imewakamata Watuhumiwa 15 wa wizi wa mtandao kupitia ujumbe mfupi wa maandishi katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dar  es salaam na mikoa ya mingine ya jirani pamoja na Rukwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam DCP- Liberatus Sabas amesema watuhumiwa hao wamekutwa na kadi 352 za mitandao mbalimbali ya simu, vitambulisho 31, Leseni, kadi za benki, Laptop 5, CPU na Moderm 2.

Watuhumiwa hao wamekiri kutumia program ya simu (Application) inayoitwa Bulk SMS ambayo ina uwezo wa kutuma meseji fupi zaidi ya 10,000kwa siku na kuzalisha namba nyingine za kupokea meseji baada ya kuweka namba ya kwanza.

LIVE MAGAZETI: ‘Watapata tabu sana’, Majina Vigogo wadaiwa yaanikwa

Soma na hizi

Tupia Comments