Mwanamume mmoja wa Japan ambaye alikaa Jela karibu nusu karne akitumikia hukumu ya kifo amegundulika kuwa hana hatia ya mauaji, Mamlaka za kisheria Nchini humo zimethibitisha.
Anaitwa Iwao Hakamada, 88, alihukumiwa kunyongwa mwaka 1968 baada ya kupatikana na hatia ya kumuua Bosi wake, Mke wake na Watoto wake wawili na kuchoma moto nyumba ya Familia yake miaka miwili baadaye.
Hakamada ambaye ni Bondia wa zamani wa ngumi za kulipwa alikaa kwa miaka 46 jela akitumikia hukumu ya kifo ambayo inaaminika kuwa ya muda mrefu zaidi katika safu ya kunyongwa kuliko Mfungwa yeyote duniani.
Bondia huyo amekuwa akipinga mara kwa mara kutokuwa na hatia na kusema kuwa Polisi wa uchunguzi walimlazimisha kukiri kosa huku Mawakili wake wakidai kuwa Polisi walikuwa na ushahidi wa kubuni.
Hakimu Mfawidhi katika Mahakama ya Wilaya ya Shizuoka, Koshi Kunii amekiri kwamba ushahidi uliotolewa dhidi ya Mfungwa huyo ulitengenezwa na ameahidi leo Alhamisi, Septemba 26, 2024 kuifuta hukumu hiyo.