Michezo

Mashabiki wa AC Milan waja na staili mpya ya kukaa uwanjani… unajua kwa sababu gani?

on

fans ac

Kutofanya vizuri kwa klabu ya AC Milan kumewafanya mashabiki wa kukasirishwa.. hii sio klabu ya kwanza kukutwa na noma ya namna hii toka kwa mashabiki.. Arsene Wenger ni moja ya makocha ambao wamepitia sana vipindi vigumu vya kukataliwa na mashabiki wa Klabu ya Arsenal, safari hii balaa limehamia AC Milan.

Wenger-despair-main

Mmiliki wa klabu hiyo Silvio Berlusconi ambaye ameiongoza klabu hiyo kwa miaka zaidi ya 30 ameonekana kuchokwa na mashabiki wa timu hiyo ambao sasa wameamua kufanya kama mgomo hivi.. wanataka mmiliki abadilishwe kwa kuwa timu haijafanya vizuri kwenye matokeo ya mechi zake nyingi walizocheza.
basta
Mashabiki hao wamekaa uwanjani kwa mtindo ambao unasomeka ‘BASTA‘ ambao tafsiri yake ni “sasa imetosha”.

Wengi wanataka kiongozi huyo aiuze klabu yake ili mtu mwingine inunue ifanye vizuri.

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments