Nyota wa Manchester United wameambiwa mustakabali wao uko kwenye mstari mwekundu katika wiki zijazo hasa karibu na dirisha la January.
Meneja mpya Ruben Amorim amesema kuwa hakuna mchezaji aliye salama kutokana na shoka la klabu.
United wako katika nafasi ya 13 kwenye Premier League na wako tayari kusafirisha majina makubwa.
Akizungumza wakati wa mkutano wake na wanahabari wiki hii, Amorim alisema: “Tuna wachezaji wazuri, tunahitaji muda wa kuwafundisha mawazo yetu kisha tutaona kwa sababu hii ni klabu kubwa.
“Kama hatutashinda, kocha anaenda, mchezaji anaenda – kwa hivyo lazima ujue hilo.”
United itamenyana na Viktoria Plzen kwenye Ligi ya Europa siku ya Alhamisi na kisha kucheza na Manchester City wikendi kwenye Ligi ya Premia.