Michezo

Amunike apoteza kazi ya Ukocha

on

Ikiwa ni mwezi mmoja umepita toka club ya El Makkasa ya Misri itangaze kuwa Mnigeria Emmanuel Amunike ndio kocha wao mpya mbadala wa Ahmed Hosam.

Leo zimetoka taarifa kwa Amunike akiwa kakamilisha mwezi leo, ameondolewa katika nafasi ya ukocha katika kikosi cha El Makkasa na kuwa mkurugenzi wa michezo wa academy za soka wa club El Makkasa Afrika nzima.

“Bado nipo ndani ya timu hakuna suala la kufukuzwa kama ilivyoripotiwa kwa sababu Makkasa ni kundi kubwa sana na mwaka uliopita walikuwa wanajaribu kutengeneza mradi mkubwa wa mchezo bara zima”- Amunike

Amunike akiwa kocha wa El Makkasa katika kipindi cha mwezi ameiongoza timu hiyo katika michezo mitatu ya Ligi akitoka sare mbili za kufungana 1-1 na kupoteza mchezo mmoja kwa kufungwa 1-0.

Soma na hizi

Tupia Comments