Top Stories

Amuua Mkewe kwa madai ya kutumia ARV kwa kificho

on

Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga linamshikilia Peter Elias (29) mlinzi na mkazi wa Ndembezi Mjini Shinyanga kwa kosa la kumuua mke wake Pili Luhende akimtuhumu kutumia Dawa za Kufubaza Makali ya Virusi vya Ukimwi (ARV) kwa kificho.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba tukio hilo limetokea May 3,2021 majira ya saa nne na nusu usiku katika mtaa wa Dome, Kata ya Ndembezi, Manispaa ya Shinyanga.

“Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga tulipokea taarifa kuwa Pili Luhende, aliuawa na Peter Elias (29), mlinzi na mkazi wa Ndembezi ambaye ni mume wake baada ya kumpiga. Baada ya taarifa hiyo mtuhumiwa alikamatwa na kuhojiwa ambapo tarehe 06/05/2021 alionyesha alipoutelekeza mwili wa marehemu maeneo ya Mwagala darajani,” Kamanda Magiligimba.

“Pia alibainisha kuwa alimpiga kwa kutumia ngumi na chanzo kikiwa ni mtuhumiwa kumbaini mkewe anatumia dawa za HIV yaani ARV kwa kificho hivyo ikamtia hasira na wamekuwa na ugomvi wa mara kwa mara kuhusiana na hilo,” Kamanda Magiligimba.

Amesema mwili wa marehemu umekutwa ukiwa umeharibika na umekabidhiwa kwa ndugu kwa taratibu za mazishi na kwamba mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

LIVE: MSEMAJI WA SERIKALI MSIGWA ANAZUNGUMZA MUDA HUU

Soma na hizi

Tupia Comments