Mtuhumiwa wa wizi amekamatwa katika Wilaya ya Kusini mwa Zimbabwe ya Gutu kwa madai ya kutumia vazi la “shetani ” kuwatisha watu anaotaka kuwaibia ili wakimbie nae aibe.
Paul Nyathi, Msemaji wa Polisi wa Kitaifa, amesema kuwa uchunguzi umethibitisha kwamba mtu huyo aliyejulikana kama Norman Chagwiza – alikuwa ameiba katika nyumba mbili.
“Angejifanya kama shetani kwa kuvalia nguo za kutishana wakati watu wanakimbia, angeiba mali zao,” Nyathi alinukuliwa akisema katika tovuti ya News Day.
“Aliiba ngazi katika nyumba fulani, kisha katika tukio lingine, alifunga mlango kutoka nje wakati akijaribu kuiba paneli za kawi ya jua , lakini mmiliki wa nyumba hiyo alivunja mlango na kumfukuza hadi akamkamata,” Nyathi