Top Stories

Anayedaiwa kubomoa nyumba ya ndugu yake, achomewa nyumba (+video)

on

Baadhi ya wananchi wa kata ya Sokoni 2 halmashauri ya Arusha jana Ijumaa Julai 9, 2021 wamechoma moto nyumba ya Ng’ida Loisulye anayedaiwa kubomoa nyumba ya ndugu yake, Benjamin Mollel kwa maelezo kuwa ameshinda kesi mahakamani.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya nyumba hiyo iliyobomolewa, Mollel amesema alishangaa kuona Polisi na madalali wakifika katika nyumba hiyo na kuibomoa kwa maelezo kuwa ameshindwa kesi mahakamani.

“Mimi nina kesi na huyu ndugu yangu muda mrefu na tulishapelekana tulianzia ngazi za chini hadi tukafika mahakamani na tulishaweka kizuizi nyumba isibomolewe na kesi ilikuwa inatajwa tena Septemba 6, 2021 sasa huyu nashangaa leo amefika hapa kuja kubomoa wakati hatuna barua wala taarifa yoyote kuhusu tukio hili,” Benjamini.

Soma na hizi

Tupia Comments