Top Stories

Angalizo lilitolewa na Wizara ya afya

on

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imewasihi na kuwasisitiza zaidi wananchi kuzingatia tahadhari zote ikiwemo uvaaji wa barakoa

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano kwa umma, Gerard Chami amesema wizara inaendelea kusimamia na kusisitiza utekelezaji wa tahadhari ya magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza na ya kuambukiza yakiwemo ya milipuko ikiwemo tishio la ugonjwa wa COVID-19.

Ametaja tahadhari zingine ikiwemo kunawa mikono, kutumia vipukusi (sanitizer),  kufanya mazoezi a, kuwalinda wale wote walio katika hatari kama wazee, watu wanene, na wenye magonjwa ya muda mrefu.

Kupata lishe bora ikiwemo matunda na mbogamboga, matumizi ya tiba asili zilizosajiliwa na baraza la tiba asili na kama inavyoelimishwa na wataalamu husika na kuwahi katika vituo vya kutolea huduma za afya mara uonapo dalili za maradhi ili watoa huduma wapate nafasi nzuri zaidi ya kutibu.

“Ni vyema kila mmoja akawa na utaratibu wa kupima afya yake mara kwa na kuendelea kuchukua tahadhari kwa kuzingatia kanuni za mtindo bora wa maisha ili kuondoa vihatarishi vya kiafya vinavyodhoofisha kinga ya mwili. Kila mmoja wetu ajione ana jukumu la kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza na yale ya kuambukiza,”  Chami.

KAKA YAKE CHIKUMBALAGA AELEZA UKWELI WOTE WA MAISHA YAO “MAMA AMEFARIKI”

Soma na hizi

Tupia Comments