Top Stories

“Angekuwa hai tungefaidika nae kwa mambo mengi, Polisi wametumia busara”- RC DSM (Video+)

on

Mkuu wa Mkoa Wa Dar es salaam, Amos Makala amepita kwenye kipindi cha Power Break Fast cha Clouds FM kuzungumzia tukio la Agosti 25, 2021 baada ya kijana mmoja kuua watu zaidi ya watatu na baadae jeshi la polisi kumdhibiti.
“Tulipongeze jeshi la polisi kwa kazi kubwa waliyofanya ya kuweza kurejesha zile silaha mbili, zile bunduki alizozipora kwa Askari wetu na bastola yake kwahiyo ingeweza kuleta madhara zaidi kama tusingeweza kuzipata hizo silaha”– RC Makalla

“Jeshi la polisi ukifuatilia wametumia mbinu kubwa ya kumrushia bomu la machozi ili atoke kwenye kile kibanda maana aling’ang’ania kwenye kile kibanda”- RC Makalla

“Angekuwa hai tungefaidika nae kwa mambo mengi, Jeshi la Polisi wametumia sana Busara na kazi kubwa”- RC Makalla

Ayo TV imekusogezea hapa video ushuhudie alichokizungumza RC Makalla kupitia Clouds FM kuhusu tukio la Majibizano ya Risasi Agosti 25, 2021

RAIS SAMIA ANENA TUKIO LA MAJIBIZANO YA RISASI DSM “MTU HUYO AMEDHIBITIWA NA HALI NI SHWARI”

VIDEO: POLISI WALIVYOFANIKIWA KUMDHIBITI MTU MMOJA AYELIKUWA ANAFYATUA OVYO RISASI DSM

Soma na hizi

Tupia Comments