Michezo

Ansu Fati avunja rekodi iliyodumu kwa miaka 22 UEFA

on

Ansu Fati usiku wa December 10 akitokea benchi dakika ya 85 kuchukua nafasi ya Carles Perez katika mchezo wa Barcelona dhidi ya Inter Milan uliyomalizika kwa Barcelona kupata ushindi wa 2-1 Ansu Fati akifunga goli la ushindi dakika ya 86 na kuandika rekodi.

Kinda wa Barcelona Ansu Fati usiku wa December 10 2019 amevunja rekodi iliyodumu kwa miaka 22 ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kufunga goli UEFA Champions League akiwa na  umri wa miaka 17 na siku 40.

Rekodi hiyo iliwekwa na Peter Ofori Quaye, October 1997 akiwa na umri wa miaka 17 na siku 194 akiichezea Rosenborg dhidi ya Olympiacos, hata hivyo Ansu Fati ana rekodi ya kuwa mchezaji wa Barcelona mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kufunga goli na watatu LaLiga kwa wenye umri mdogo kuwahi kufunga goli LaLiga.

Soma na hizi

Tupia Comments