Michezo

Anthony Joshua imethibitika anapanda ulingoni June 20

on

Wakati kukiwa na habari kuwa mapromota wako mbioni kumshawishi apokee pesa bondia Deontay Wilder ili amuache Tyson Fury akacheze na muingereza mwenzake Anthony Joshua na sio kucheza pambano la tatu la marudiano.

Bondia Anthony Joshua imethibitika kuwa atapanda ulingoni June 20 katika uwanja wa Tottenham kwa ajili ya kupambana na  bondia Kubrat Pulev.

Joshua ambaye anakaribia miaka miwili hajapanda ulingoni katika ardhi ya Uingereza atapanda ulingoni katika ardhi ya kwao June 20 kutetea mikanda yake ya IBF, WBO na WBA uzito wa juu, mara ya mwisho kupigana katika ardhi ya England ilikuwa mwaka jana katika uwanja wa Wembley dhidi ya Alexander Povetkin.

Soma na hizi

Tupia Comments