Duniani

Hii ndio kali yenyewe, unakojolea ukuta alafu mkojo unakurudia mwenyewe (+Video)

on

Kama una tabia ya kujibana kona alafu unajisaidia haja ndogo, mambo yanaweza kukuharibikia kona yoyote !!

Nasubiri kuona hii kitu kwa hamu sana, itapunguza matangazo yaliyoandikwa ‘USIJISAIDIE HAPA, UKIKAMATWA FAINI ….

Hii stori nimeipata kwenye ukurasa wa BBC mtandaoni, wamesema Uingereza wako kwenye majaribio ya rangi maalum ambayo haipatani na mkojo kabisa, ikitokea mtu kajibana kujisaidia kwenye ukuta wenye rangi hiyo basi mkojo wote unamrudia mwenyewe !!

London ndio hivyo wameshaamua, na kilichowakasirisha zaidi ni kwamba wamekuwa wakitumia karibu pound 100,000 (kama Tshs. Milioni 318) kwa ajili ya kusafisha kuta ambazo zimekojolewa pamoja na mikojo iliyotuama barabarani, dawa inakuja aisee..

Hapa nina kipande cha video kutoka Ujerumani, miezi 9 iliyopita nao waliwahi kuamua kupaka rangi hiyo kukomesha walevi na wapita njia mabingwa wa kujisaidia kwenye kuta za mitaani.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments