Michezo

Antonio Conte kaeleza sababu za Sanchez kukaa benchi

on

Kocha wa Inter Milan Antonio Conte ameeleza kuwa hakupandwa na uazimu kufanya maamuzi ya kumuacha benchi mshambuliaji wake Alex Sanchez, Conte amesema mchezaji huyo anatatizo na utimamu katika mwili wake (fitness).

Majeruhi yamekuwa yakimchelewesha sana Sanchez kurudi katika ubora wake kama ambavyo wengi wamemzoea, Sanchez hadi sasa amecheza game Italia na kuumia mguu ambapo kumemfanya akae nje hadi mwaka mpya 2020.

“Wachezaji wanatakiwa kuwa vizuri vinginevyo huo utakuwa ni wazimu (kutomchezesha) au nitakuwa mjinga ama nitakuwa nataka kujiumiza mwenyewe, kama moja jumlisha moja inakuwa mbili, halafu ukitaka kupata tano? (lazima uongeze mchezaji), kama simchezeshi mchezaji sio kwa sababu nimepata wazimu kuna sababu”>>>Antonio Conte

VIDEO: KUMLAUMU AISHI MANULA NI KUMKOSEA HESHIMA BALAMA WA YANGA

Soma na hizi

Tupia Comments