Habari za Mastaa

Kim Kardashian atinga Ikulu ya Trump kumpigania Asap atoke jela

on

Mwanadada Kim Kardashian ameonekana kupigania haki za wafungwa nchini Marekani na hadi kufikia hatua ya kuwasaidia wengine kuachiwa huru sasa kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Kim pamoja na mumewe Kanye West wako njiani kumsaidia rapper Asap Rocky.

Rapper huyo ambaye kwa sasa yupo jela nchini Sweden, Kim na Kanye wako mbioni kumsaidia huku ikiwa imeelezwa kuwa wawili hao walikuwa kwenye mazungumzo na Ikulu ya Marekani kwa ajili ya mchakato mzima wa kesi inayomuandama Asap Rocky.

Kwa mujibu wa watu wa karibu waliuambia mtandao wa TMZ kuwa Kim alifanya mazungumzo ya simu na mkwe wa Trump ambaye ni Jared Kushner na alimuelezea kuhusu kesi ya Asap na hivyo mwanamama huyo alifikisha taarifa hiyo Ikulu kwa ajili ya majadiliano.

Siku kadhaa zilizopita baada ya Asap Rocky kukamatwa Snoop Dogg alitoa tamko kwa Kim na kumtaka amsaidie rapper huyo kama ambavyo aliwasaidia wafungwa wengine kutolewa gerezani na kuwa huru. Rapper Asap Rocky alikamatwa June 30,2019 mitaa ya Stockholm, Sweden baada ya kuanzisha ugomvi na kusababisha kukosekana kwa utulivu eneo hilo.

VIDEO: ULIPITWA NA HII YA MASTAA WAKIWA KWENYE SURA YA KIZEE? BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

Soma na hizi

Tupia Comments