Leo January 8, 2018 nimeipata hii kutoka Falme za Kiarabu ambapo Wanawake wataruhusiwa kuanzia mwezi huu kuhudhuria kwenye michezo ya kandanda ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya Saudi Arabia.
Maafisa wa Saudi Arabia wamesema kuwa mashabiki wa kandanda wanawake wataanza kuingia katika viwanja vya mpira katika taifa hilo kuangalia michezo mitatu inayohusisha timu zinazoshiriki ligi ya nchi hiyo katika mechi ya Ijumaa, Jumamosi na January 18, 2018.
October 2017, idara inayohusika na masuala ya michezo ya Saudi Arabia ilitangaza kufikia 2018 viwanja vitatu ambavyo vilikuwa vinatumika na wanaume tu vitaandaliwa kwa ajili ya kutumiwa pia na wanawake ikiwa ni pamoja na kuwa na maeneo maalumu ya kukaa.
Mwana wa Mfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman ameondoa marufuku ya wanawake kujihusisha na mchezo wa kandanda, wakati akijaribu kurudisha heshima ya nchi hiyo kimataifa.
GOOD NEWS ALIYOITANGAZA MBWANA SAMATTA LEO