Baada ya Benki Kuu ya Tanzania kuzifunguia benki tano January 4, 2018 ikiwemo Meru Community Bank baadhi ya wateja wa benki hiyo wameiomba serikali kuwasaidia kupatikana kwa fedha walizokuwa wameweka katika benki hiyo ili ziweze kuwasaidia katika matumizi mbalimbali.
Mmoja wa wateja aliyejitambulisha kwa jina la Elizabeth Munish amesema yeye aliwekeza pesa zake kwenye benki hiyo kwa sababu aliamini ni Benki ya wananchi na ni sehemu salama kuweka pesa zake na hivyo taarifa ya kugungiwa ameipokea kwa masikitiko makubwa.
“Nimeweka pesa nyingi, ada za watoto zote nilikuwa nimeweka huku, hata Jumatatu sina ada ya kuwapeleka wanangu shule, nina watoto wa chuo na wa shule za English medium, sina hata senti tano na ndani nia shilingi Elfu ishirini tu.” – Elizabeth Munish
Muhimbili Hospitali wazungumzia Hali ya Mzee Kingunge
MAHAKAMANI: Rugemarila amewataja ‘wezi wa fedha za Escrow’