Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo Desemba 10 2016, amekutana na kufanya mazungumzo na Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara, Alhaji Aliko Dangote.
Rais Magufuli amekutana na Dangote ambaye kwa mujibu wa jarida la Forbes ndio bilionea namba moja Afrika, ameongea na kumuhakikishia mazingira mazuri kwa uwekezaji wake na wawekezaji wote waliopo na watakaokuja Tanzania.
VIDEO: Ulikosa kutazama taarifa ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji kuhusu wawekezaji sita wanaotaka kuondoka Tanzania? Tazama hapa chini