AyoTV

Polisi Arusha yaeleza sababu za kuwashikilia Askari 6 wa SUMA JKT

on

Tukio la mauaji ya watu wanne ndani ya siku moja yaliyotokea Arusha Tanzania limefanya waliohusika na mauaji hayo ambao ni Askari wa SUMA JKT kukamatwa na Polisi Arusha na uchunguzi unaendelea.

Kilichotokea ni kwamba Mifugo ya Wafugaji wanaoishi karibu na msitu wa Oldonyosambu Arumeru Arusha iliingia kwenye eneo ambalo linalindwa na Askari hao ambapo mwanzoni Mifugo 45 iliingia na kukamatwa.

Baadae mifugo mingine 80 tena ikaingia kwenye eneo hilo kwa ajili ya kula majani ambapo Askari hao waliikamata na ndipo fujo zikatokea pale Wafugaji wa Kimasai wakiwa na silaha zao walipokataa mifugo yao kuchukuliwa.

Kwenye mapigano hayo Wafugaji wanne wamepoteza maisha papohapo kwa kupigwa risasi na watano wamejeruhiwa  ambapo Kamanda wa Polisi Arusha Charles Mkumbo amesema Askari sita wa SUMA JKT wanashikiliwa na Polisi na uchunguzi unafanyika ili kufahamu kama walitumia nguvu isiyostahili kwenye tukio hilo.

Kwenye hii video hapa chini Utamsikia Kamanda akiongea pamoja na mmoja wa waliojeruhiwa akisimulia ilivyokua.

Soma na hizi

Tupia Comments