Chama cha soka Argentina (AFA) kimetangaza kuahirisha mechi zote za soka zilizokuwa zichezwe leo Ijumaa ya September 2 2022 kutokana na kufeli kwa jaribio la shambulio la mauaji ya Makamu wa Rais wa Taifa hilo Cristina Fernandez de Kirchner (69).
Maamuzi hayo yamekuja baada ya shambulio hilo kuonekana ni tishio kwa usalama wa nchi, ambapo limetokea wakati Cristina Fernandez anarejea nyumbani kwake akitokea Mahakamani Buenos Aries ambapo amekana mashtaka ya tuhuma za rushwa zinazomkabili.
Tukio hilo limetokea alhamisi kwa mwanaume mwenye umri wa miaka 35 Raia wa Brazil kutoa bastola na kutaka kumfyatulia risasi lakini bastola iliyokuwa na risasi tano iligoma na jaribio hilo kufeli na kujikuta akiishia mikononi mwa Polisi.
Bi Cristina Fernandez de Kirchner ni makamu wa Rais wa 37 wa Argentina toka 2019 na amewahi kuwa Rais wa 54 Argentina toka 2007-2015, na alikuwa mke wa Rais wa Argentina Néstor Kirchner aliyedumu madarakani 2003-2007 kisha mkewe kuchukua nchi.