Michezo

Wafikishwa Mahakamani kwa kuvujisha video za mwili wa staa wa soka uliyokuwa mochwari

on

Mkurugenzi wa kampuni ya CCTV na muajiriwa wake wamejikuta wakiingia matatizoni baada ya kubainika kuwa wamevujisha picha za mochwari za mwili uliokuwa umeharibika wa marehemu Emiliano Sala.

Emiliano Sala alifariki katika ajali ya ndege ndogo binafsi akitokea Nantes kwenda Cardiff kuungana na wachezaji wenzake wapya baada ya siku chache nyuma kukamilisha usajili huo na alikuwa amerudi Nantes FC kuaga wachezaji wenzake.

Emiliano Sala

Sherry Bray mwenye umri wa miaka 49 na muajiri wake Christopher Ashford mwenye umri wa miaka 62, wamefikishwa mahakamani kwa kosa la kuvujisha video za mwili wa marehemu Emiliano Sala ambaye alifariki na mwili wake kutafutwa hadi kupatikana kwa zaidi ya siku 10.

 

Soma na hizi

Tupia Comments