Michezo

Kuhusu Robben kuongeza mkataba mpya na Bayern.

on

Borussia Dortmund v FC Bayern Muenchen - UEFA Champions League FinalWinga wa kimataifa wa Uholanzi anayekipiga Bayern Munich Arjen Robben ameongeza mkataba wake kwa miaka miwili ambapo hii imethibitishwa na klabu yenyewe.

Robben ambae alihamia Munich akitokea Real Madrid mwaka 2009, amekuwa na mafanikio kwenye hii club huku wakitwaa makombe ya ndani na nje ya Ujerumani ambapo alifunga bao la ushindi la Bayern katika fainali ya Champions League dhidi ya  Borussia Dortmund katika dimba la Wembley.

“Nipo hapa kwa mwaka wangu wa tano na miaka mingine mitatu ya kuendelea na Bayern zaidi, naangalia mbele katika miaka mingine iliyobakia kuitumikia klabu na kushinda makombe mengi zaidi” hayo ni maneno ya Robben.

 

Tupia Comments