Kocha mkuu wa Liverpool Arne Slot amesema anatumai kuendelea kufanya kazi na nahodha Virgil van Dijk “kwa muda mrefu” huku kukiwa na sintofahamu juu ya mustakabali wa muda mrefu wa beki huyo.
Van Dijk, pamoja na wachezaji wenzake Mohamed Salah na Trent Alexander-Arnold, mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu na sasa yuko huru kuzungumza na vilabu vya ng’ambo kuhusu kusaini makubaliano ya awali ya mkataba wa kujiunga na uhamisho wa bure msimu wa joto.
Hata hivyo, bado kuna matarajio huko Anfield kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 atakabidhi mustakabali wake kwa vinara hao wa Ligi ya Premia, huku kiwango chake cha kuvutia kikiwa hakionyeshi dalili za kudidimia.
“Virgil anastahili kila pongezi anazopata,” Slot aliambia mkutano wa wanahabari siku ya Ijumaa. “Amekuwa bora kwa klabu hii kwa miaka mingi na, tangu niwe hapa, amekuwa bora kwangu pia.