Michezo

Arnold aondolewa kwenye kikosi cha England Euro 2020

on

Beki wa kulia wa Liverpool Alexander Arnold ameondolewa kwenye kikosi cha England kitachoshiriki michuano ya Euro 2020 kutokana na kupata majeraha ya mapaja katika mchezo wa kirafiki wa jana wa England dhidi ya Austria.

Arnold alikuwa na hati hati ya kutoitwa katika kikosi cha England kwenye michuano ya Euro toka awali ila majeraha sasa yanamuondoa rasmi kutokana na kuwa atahitajika kujiuguza kati ya wiki nne hadi sita.

Michuano ya Euro 2020 inatarajia kuanza June 11 kwa mchezo wa ufunguzi kati ya Italia na Uturuki, England wakiwa Kundi D kenye timu za Croatia, Czech Republic na Scotland.

 

Soma na hizi

Tupia Comments