Magazeti

Ilikuwa ni Chelsea VS Arsenal kwenye ngao ya hisani, matokeo yalikupita?

on

Pazia la ligi kuu ya England limefunguliwa leo rasmi kwa mchezo wa kugombea taji la ngao ya hisani ya FA, mechi ambayo inawakutanisha washindi wa kombe la Barclays Premier League na mshindi wa kombe la FA au League Cup.
 Mchezo wa Ngao ya hisani mwaka huu umewakutanisha mahasimu wa jiji la London , Klabu Chelsea dhidi ya Arsenal, na matokeo ya mchezo huo ni ushindi kwa vijana wa Arsene Wenger.
Goli la ushindi lilofungwa kipindi cha kwanza na Alexander Chamberlain lilitosha kuwapa Arsenal ushindi muhimu dhidi ya Chelsea.

Pia siku ya leo imekuwa nzuri kwa kocha Wenger ambaye leo ndio mara ya kwanza ameweza kupata ushindi dhidi ya timu anayoiongoza Jose Mourinho.

Ligi Kuu ya Uingereza itaanza rasmi wikiendi ijayo.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments