Newcastle kwa muda mrefu wamekuwa wakihusishwa kutaka kumnunua kiungo wa Al Hilal, Ruben Neves, lakini TalkSPORT inadai kuwa wanaweza kukabiliwa na ushindani kutoka kwa Arsenal.
Neves, 25, alihamia Saudi Arabia kutoka Wolves kwa takriban £60m msimu wa joto. Lakini Newcastle wanahitaji bima ya Sandro Tonali aliyepigwa marufuku na wamekuwa wakiangalia uwezekano wa kutumia uhusiano wao na Mfuko wa Uwekezaji wa Umma wa Saudi Arabia (PIF) kumsajili kwa mkopo.
Ligi ya Premia inaweza kuzuia vilabu vinavyotoa wachezaji kwa mkopo kutoka katika kundi lao la umiliki, kama Newcastle wangefanya, hivyo Arsenal wanaweza kuchukua nafasi ya Thomas Partey aliyejeruhiwa.