Premier Bet SwahiliFlix Ad Halotel Ad

Michezo

Arsenal wafanya mauaji kwenye EPL.

on

ARSENAL

 

Washika bunduki toka jijini London Arsenal hii leo (jumapili) wamefanikiwa kuwafunga Aston Villa kwa ushindi mnono wa 5-0 katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Emirates katika muendelezo wa ligi kuu ya England .

Arsenal walianza mchezo huo kwa kasi wakifunga bao la haraka kwenye dakika ya 8 mfungaji akiwa mshambuliaji raia wa Ufaransa Olivier Giroud baada ya pasi ya beki Per Mertersecker .

Arsenal walifunga bao la pili kupitia kwa kiungo mshambuliaji Mesut Ozil ambaye alipokea pasi ya Giroud na kuukokota mpira kabla ya kupiga shuti dogo lililompita kipa wa Aston Villa Brad Guzan .

Mshambuliaji Olivier Giroud akiifungia Arsenal bao la kwanza kwenye mchezo wa leo .

Mshambuliaji Olivier Giroud akiifungia Arsenal bao la kwanza kwenye mchezo wa leo .

Theo Walcott aliifungia Arsenal bao la tatu kwenye dakika ya 63 baada ya kupewa pasi na Santi Cazorla ambaye alikuwa moja kati ya wachezaji waliong’aa katika mchezo wa leo .

Bao la nne lilifungwa kwa njia ya penati baada ya kipa wa Aston Villa Brad Guxzan kumchezea vibaya mshambuliaji chipukizi Chupa Akpom , Santi Cazorla alipiga penati hiyo na kuipa timu yake bao linguine huku Aston Villa wakiendelea kupata wakati mgumu .

Theo Walcott alifunga bao la pili kwenye mchezo dhidi ya Aston Villa.

Theo Walcott alifunga bao la tatu kwenye mchezo dhidi ya Aston Villa.

Wakati mchezo ukielekea mwishoni , beki wa kushoto Hector Bellerin alifunga karamu ya mabao baada ya kuipa Arsenal bao la tano .

Ushindi huu unawafanya Arsenal kuchupa hadi nafasi ya tano wakiwa na pointi 42 , pointi moja nyuma ya Man United walioko kwenye nafasi ya nne .

Kiungo  Mesut Ozil naye alikuwa moja ya wafungaji .

Kiungo Mesut Ozil naye alikuwa moja ya wafungaji .

Tupia Comments