Michezo

Arsenal waiadhibu Man City hao fainali

on

Club ya Arsenal leo imecheza game ya nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Man City katika uwanja wa Emirates.

Mchezo huo ambao mshindi ndio alikuwa anatinga kucheza fainali ya FA Cup, Arsenal walifanikiwa kushinda 2-0 kwa magoli yaliofungwa na Pierre Emerick-Aubameyang dakika ya 19 na 71.

Mvuto wa mchezo huu ulikuwa zaidi kwa makocha wa timu hizo ambapo kocha wa Man City Pep Guardiola alikuwa anakutana na Kocha wa Arsenal Mikel Arteta ambaye ni msaidizi wake wa zamani.

Soma na hizi

Tupia Comments