Michezo

Arsenal wamemtema Mesut Ozil

on

Kiungo wa Arsenal Mesut Ozil ambaye ndio mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi katika kikosi cha Arsenal, leo imetangazwa rasmi na club hiyo kuwa ameachwa katika kikosi cha wachezaji 25 wa Arsenal watakaoshiriki Ligi Kuu England 2020/21

Taarifa hizo zinakuwa pigo zaidi kwa Ozil ikiwa ni wili chache zimepita toka Arsenal chini ya kocha wao Mikel Arteta watangaze kumuacha tena katika kikosi cha Arsenal kitakachoshiriki katika michuano ya UEFA Europa League 2020/21.


Ozil amekuwa akicheza katika mechi zote za Arsenal chini ya Mikel Arteta hadi mwezi March kabla ya Ligi haijasimama lakini hadi sasa toka March hajapewa nafasi ya kucheza ukiwa mkataba wake unaelekea ukingoni mwisho wa msimu 2020/21.

Arsenal pia wamemkata beki Sokratis katika kikosi chao, sasa ni wazi kwa kuwa dirisha la usajili limefungwa wachezaji hao watacheza katika vikosi vya Arsenal vya U-23 ili kulinda viwango vyao.

Arsenal hadi sasa katika timu yao wako na wachezaji 19 walio zaidi ya umri wa miaka 21 ambao sio vipaji vilivyokulia hapo, yaani ni wawili zaidi wameongezela  wanaoruhusiwa na UEFA hivyo Sokratis na Ozil ndio wamepunguzwa.

Soma na hizi

Tupia Comments