Michezo

Arsenal ya Arteta yatamba na makinda FA

on

Club ya Arsenal leo ilikuwa ugenini kucheza game yake ya FA dhidi ya wenyeji wao AFC Bournemouth, mashabiki wakiwa na matarajio makubwa ya ushindi kufuatia ubora wa Arsenal ukilinganisha na Bournemouth.

Arsenal inaonekana walikuwa na tahadhari zaidi ukilinganisha jana vigogo wenzao Liverpool walikutana na ugumu dhidi ya Shrewsbury  ya Ligue One na kujikuta wakitoka sare ya 2-2.

Leo Arsenal wamepata ushindi wa magoli 2-1, magoli ya Arsenal yakifungwa na Bukayo Saka dakika ya 5 na Eddie Nketiah dakika ya 26 katika uwanja wa Vitality huku Bournemouth wakijipoza kwa bao pekee lililofungwa na Sam Surridge dakika za nyongeza.

Soma na hizi

Tupia Comments