Michezo

Arsenal yaendelea kutamba FA Cup

on

Club ya Arsenal ya England imeendelea kuwa na wakati mzuri katika michuano ya FA Cup wakati huu wakiwa na hali ngumu juu ya hatma yao katika EPL kama watafanikiwa walau kupata nafasi ya kucheza Europa League.

Leo Arsenal imecheza game ya round ya tano ya FA Cup dhidi ya Portsmouth na kufanikiwa kusonga mbele kwa kupata ushindi wa magoli 2-0.

Magoli ya Arsenal yakifungwa na Sokratis dakika ya 45 na Nketiah aliyefunga la pil dakika ya 51, kocha wa Arsenal Mikel Arteta licha ya kutokuwa na matumaini ya taji lolote lakini mchezo huu hakuwatumia kwa kiwango kikubwa wachezaji wake wa kikosi cha kwanza.

Soma na hizi

Tupia Comments