Winga wa Kimataifa wa Ubelgji Leandro Trossard (28) amejiunga na club ya Arsenal wa akitokea Brighton.
Trossard ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha Ubelgiji kilichocheza World Cup 2022 nchini Qatar, msimu huu ameifungia Brighton goli 7 katika michezo 16.
Trossard anajiunga na Arsenal na sasa atakuwa akilipwa mara mbili ya mshahara wake akiwa Brighton, jezi namba 19 iliyokuwa inatumiwa na Nicolas Pepe ndio ataivaa Trossard.