Michezo

Arsenal yasajili nyota wa Brazil.

on

gabriel paulista

 

Klabu ya Arsenal iko mbioni kukamilisha usajili wa nyota raia wa Brazil Gabriel Paulista toka kwenye klabu ya Villareal ya nchini Hispania .

Usajili huu utakamilika siku chache zijazo baada ya mchezaji huyo kupata kibali ch akufanyia kazi nchini England kulingana na sheria za kazi kwa raia wanaotoka nje ya umoja wa ulaya .

Beki huyo mwenye umri wa miaka 24 anatarajiwa kukamilisha vipimo vya afya hii leo (jumatatu) na atakamilisha usajili wake baada ya hapo .

Gabriel Paulista atajiunga na Arsenal muda wowote kuanzia sasa.

Gabriel Paulista atajiunga na Arsenal muda wowote kuanzia sasa.

Awali kulikuwa na hofu kuwa Paulista angenyimwa kibali cha kufanyia kazi kwa kuwa hajacheza mechi zozote za kimataifa lakini hiyo haitakuwa shida kwani ameichezea klabu ya Villareal kwa muda mrefu na amekidhi vigezo vya kupata kibali cha kufanyia kazi nchini humo .

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amethibitisha hili ambapo amesema kuwa dili la kumsajili beki huyo litakamilika muda wowote kuanzia sasa .

Paulista aligana na wachezaji wenzie wa Villareal dakika chache kabla ya mchezo dhidi ya Levante kwenye ligi ya Hispania huku pia akitumia fursa hiyo kuagana na mashabiki.

Mshambuliaji wa Costa Rica Joel Campbell ameruhusiwa kujiunga na Villareal kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu huu kama sehemu ya usajili wa Gabriel Paulista.

Mshambuliaji wa Costa Rica Joel Campbell ameruhusiwa kujiunga na Villareal kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu huu kama sehemu ya usajili wa Gabriel Paulista.

Katika mchakato wa kumsajili Paulista Arsenal imemruhusu mshambuliaji raia wa Costa Rica Joel Campbell kujiunga na Villareal kwa muda wote uliobaki wa msimu huu .

Tupia Comments