Michezo

Isikie hii kauli ya mashabiki wa Arsenal kwa nahodha wao wa zamani Cesc Fabregas!!

on

fabVinara wa ligi kuu England wanakutana na wababe wengine wa ligi hiyo Arsenal mwishoni mwa juma hili katika uwanja wa Emirates  ikiwa ni harakati za kuwania ubingwa wa ligi hiyo.

Lakini kauli ya mashabiki wa Arsenal kwa nahodha wao wa zamani Cesc Fabregas ambaye kwa sasa anaichezea Chelsea inaweza kukuchekesha kwani wameutaka uongozi wa klabu hiyo kuondoa bango lenye picha ya staa huyo kwenye uwanja wao.

Mashabiki hao wamesisitiza ni lazima bango hilo liondolewe kabla ya mchezo wao jumapili kwa kuwa Fabregas anarudi kwenye uwanja huo akiwa mpinzani wao mkubwa.

Fabregas raia wa Hispania aliichezea Arsenal kwa mafanikio makubwa kabla ya kuondoka mwaka 2011 na kujiunga na Barcelona lakini akarejea England na kujiunga na Chelsea ambayo sasa inapambana na Arsenal katika kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England jumapili hii.

Hakuna Stori itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments