Michezo

Maamuzi ya Arsene Wenger kwa Man United saa kadhaa kabla ya dirisha la usajili halijafungwa …

on

Kocha wa klabu ya Arsenal ya Uingereza Arsene Wenger February 1 tukiwa tunaelekea kufungwa kwa dirisha dogo la usajili la mwezi January, ameingia kwenye headlines baada ya kugoma kumuacha beki wa kimataifa wa Ufaransa anayeichezea klabu hiyo Mathieu Debuchy kujiunga na klabu ya Man United kwa mkopo.

Wenger anatajwa kukubali kumruhusu beki huyo aende klabu ya Bordeaux, maamuzi ambayo yamesababishwa na Mathieu Debuchy mwenye ambaye anahitaji kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara ili aweze kuitwa kucheza michuano ya Euro 2016 katika timu yake ya taifa ya Ufaransa.

DONETSK, UKRAINE - JUNE 15: Mathieu Debuchy of France controls the ball during the UEFA EURO 2012 group D match between Ukraine and France at Donbass Arena on June 15, 2012 in Donetsk, Ukraine. (Photo by Julian Finney/Getty Images)

Beki huyo wa kulia wa Arsenal mwenye umri wa miaka 30 alikuwa katika rada za kocha wa Man United Louis van Gaal ambaye anatajwa kuwa na tatizo la uimara wa ngome yake ya ulinzi. Wenger amekataa kumruhusu beki huyo ajiunge na Man United kwa sababu ya vilabu vingi vya Uingereza huwa havipendi kumuuza mchezaji katika timu mpinzani,

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments