Uongozi wa Arsenal kupitia kwa mtendaji mkuu wake inadaiwa kumfanyia interview kiungo wa zamani wa timu hiyo Mikel Arteta kwa ajili ya kumpa kibarua cha kuinoa Arsenal, kwa sasa Arsenal wanamtazama Arteta kama mbadala sahihi wa timu yao baada ya mbinu za Arsene Wenger na Unai Emery kufeli.
Awali iliripotiwa na mitandao mbalimbali ya michezo kuwa uongozi wa Arsenal ulikwenda nyumbani kwa Arteta usiku na kufanya nae mazungumzo ya kina, kabla ya kupeleka ofa mezani kwa Man City kuwa wanataka kuvunja mkataba wa Arteta na Man City wa ukocha usaidizi ili ajiunge na Arsenal.
Hata hivyo Arteta mwenye umri wa miaka 37 alikuwa ni chaguo la kwanza kama mrithi wa Wenger baada ya Arsenal kuamua kuachana na Wenger 2018, Arteta aliondoka Arsenal 2016 kama mchezaji na kujiunga na Man City kama kocha.
VIDEO:PAMBANO LA ROUND 10: MWAKINYO VS TINAMPAY