Kutunza afya ni kitu muhimu kwa kila mtu, mara nyingine huwa inatokea tu tunajisahau kwenye ishu ya afya.. leo nimekumbushwa kitu muhimu sana, nilikuwa mmoja ya watu waliohudhuria kwenye Semina ya ‘Afya Bora ni Msingi wa Mafanikio ya Sanaa Yako’ ambayo ilikuwa ikitolewa na Dr. Mwaka DAR.
Wasanii wengi walikuwepo kwenye semina hiyo, najua Semina hiyo itakuwa imewapa somo kubwa sana wasanii hao juu ya ishu ya kutunza na kulinda afya zao.
Dr. Mwaka ametoa Semina kwa wasanii kuwa makini kutunza afya, kujilinda na kuwa na tabia ya kupima afya zao ili kujiweka sawa wakati wote.