AyoTV

VIDEO: Wafanyabiashara Arusha wapinga kuondoka kwenye maduka, Meya azungumzia hilo

on

Leo January 17 2017 kutokea Arusha ni kwamba wafanyabiashara wa jiji hilo wamepinga  kupewa notisi ya miezi mitatu kuondoka katika maduka 1135 kwa madai ya kushiriki katika ujenzi wa maduka hayo.

Awali agizo la halmashauri ya jiji hilo liliwataka kuondoka ili waweze kutangaza tenda mpya itakayowezesha halmashauri kuongeza mapato kupitia maduka hayo. AyoTV  imezungumza na wafanyabiashara hao pamoja na Meya wa jiji hilo.

Wakizungumza na millardayo.com na Ayo TV, Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara hao Lonken Massawe amedai kuwa wanalipa zaidi ya milioni 200 kwa maduka ya stand ndogo, soko kuu pamoja na soko la kilombero na hawajakataa mazungumzo na halmashauri.

Baada ya malalamiko hayo MillardAyo.com na Ayo TV imempata pia mstahiki meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro ambapo amesema…..>>>wanafanya siasa kwenye mali ya umma, Lonken ametajwa kwenye ripoti ya CAG kwamba ni moja ya watu wanoihujuumu halmashauri na ametajwa kwenye ukurasa wa 48, ni mmoja wa wafanyabiashara ambao wamesababisha halmashauri hii kupoteza Bil 2.1′

VIDEO: Ombi la wasafirishaji wa viumbe hai baada ya kupigwa marufuku, Bonyeza play hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments