Rais wa awamu ya tano wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Joseph Magufuli amezungumza na wananchi wa Arusha wakati wa uwekwaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi wa barabara ya njia nne kwa mara ya kwanza Arusha.
Hafla ya uwekwaji wa jiwe la msingi lililowekwa na Rais Magufuli na Rais Uhuru Kenyata wa Kenya katika eneo la Tengeru Arusha ulihudhuriwa na viongozi wengine wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kama Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Makamu wa Rais wa Burundi Dk Joseph Butore.
Kwa upande wa Tanzania ujenzi huo utatekelezwa kwa awamu mbili, kwanza ujenzi wa njia nne kutoka Arusha hadi Tengeru yenye urefu wa Kilometa 14.1, ujenzi wa barabara ya mzunguuko “Bypass” yenye urefu wa Kilometa 42.4.
Wakati awamu ya pili ni ujenzi wa njia nne kuanzia Tengeru hadi Usa River yenye urefu wa Kilometa 8.2 na Usa River hadi Holili mpakani mwa Kenya na Tanzania yenye urefu wa Kilometa 100.2
“Nachoweza kusema ni kwamba nawashukuru kuja kwa wingi kushuhudia uwekwaji wa jiwe la msingi, kwa barabara inayotoka Arusha, Holili, Taveta na Voi yenye jumla ya Kilometa 234.3 ambayo inajengwa” >>> Rais Magufuli
Unaweza kusikiliza hapa maneno ya Rais Magufuli
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE