Baada ya habari za winga wa klabu ya Azam FC Farid Musa kuendelea kuwa Dar es Salaam kwa vigezo vya kusubiri vibali vipatikane katika klabu ya Tenerife ya Hispania, kumekuwa kuna habari nyingi zikiandikwa kuwa Azam FC hawataki kumuuza na wengine wakisema kuna mtu nje ya Azam FC anajaribu kukwamisha dili hilo, CEO wa Azam FC Saad Kawemba kaamua kulitolea ufafanuzi.
“Suala la Farid kwanza inasikitisha watu kufikiria kuwa Farid atacheza Tanzania, mwenye mawazo hayo naomba ayafute, Azam FC tayari tumetoa ITC ya Farid ipo Tenerife ya Hispania, tatizo ni suala la kibali chake cha kufanya kazi na kinashughulikiwa na Tenerife, Farid anaenda kucheza Tenerife kwa mkopo hajauzwa”
ALL GOALS: Yanga vs Simba October 1 2016, Full Time 1-1