Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema amemteua aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe kwakuwa Chongolo anaijua vizuri Songwe.
Akiongea Ikulu Dar es salaam leo March 13,2024 wakati akiwaapisha Viongozi mbalimbali, Rais Samia amesema “Mh. Chongolo tunakupeleka Songwe, Songwe unaijua vizuri ukiwa Chamani (CCM) nimekupeleka wewe najua Songwe unaijua vizuri kwahiyo utakwenda kutuwakilisha vizuri lakini Songwe inatuunganisha na Zambia kuna Tunduma pale ambako kuna mambo mengi ya kiuchumi yanayotokea Tunduma na hivyo uhalifu wengi wa kiuchumi upo Tunduma ikiwemo ukwepaji kodi, ubadilishanaji wa fedha isivyo halali mambo mengi yanatokea pale”
“Una DED wa upande ule mzuri kidogo ameweza kuongeza mapato ya Serikali kwahiyo nenda kasaidianae nae mfanye kazi vizuri, pale Tunduma panaweza kuendesha Mkoa na mkachangia vizuri Serikali yetu kwahiyo nenda kasimamie vizuri, kuna matatizo ya TRA na nani nenda kawasaidie ili wafanye kazi zao vizuri wakiwa pale”