Habari za Mastaa

Familia yamzuia Banza Stone? Asha Baraka kaongea

on

.

.

Wengi tunafahamu kuwa muimbaji wa longtime kwenye muziki wa dance, Banza Stone anaumwa sasa leo millardayo.com ilimtafuta Mkurungezi wa kampuni ya ASET, ambaye ni mmiliki wa bendi ya African Stars aka Twanga Pepeta Asha Baraka kuzungumza machache kuhusu Banza Stone.

Akizungumza na millardayo.com alisema..‘Kikubwa zaidi ni kuhusu Banza Stone, mimi mwenyewe niliwahi kumpeleka banza mara mbili Hospitali, mara ya kwanza ilikuwa ni Muhimbili baadae nikampeleka Mwananyamala huko ndio kuna msaada wa Ma Daktari lakini this time imekuwa tofauti ambapo familia yake ina muuguza Nyumbani, kuuguzwa nyumbani kwamba anapelekwa hospitali hizi za kawaida kisha anapewa dawa anamezea nyumbani inakuwa pia ni tatizo kwa hiyo watu watahisi kuwa sisi wasanii tunamtenga au hatukwendi nyumbani kumjulia hali yake

Hata Juzi nilijaribu kuwashawishi wenzangu marafiki ambao ni wa karibu wakaongee na mama Banza ili Banza Stone aweze kwenda hospitali kwasababu mimi mwenyewe niliende ila sikuweza kufanikiwa kumpeleka hospitali halafu nashindwa kumchukua mgonjwa akiwa ndani ya familia kumpeleka hospitali kwani lolote linaweza likatokea kwa hiyo watu wasione kama sisi tunamtenga Banza kuna ugumu pale namna kumtoa Banza kumpeleka hospitali lakini tunaomba kama kuna mtu yoyote ana nguvu basi atusaidie kumchukua Banza ampeleka hospitali..’alisema

Unataka kumsikiliza Asha Baraka alichokizungumza? bonyeza play kwa chini

Jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>> Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments