Top Stories

Mwanaume auawa kwa kuchomwa visu akiamulia ugomvi wa wanandoa….Ilikuwaje?

on

Mwanaume mmoja Mjini Mombasa Kenya ameuawa kwa kuchomwa visu vingi mfululizo baada ya kuingilia ugomvi wa wanandoa waliokuwa wakipigana ndani ya nyumba yao ili amsaidie mwanamke ambaye ndiye alikuwa akipigwa.

Inaelezwa kuwa wanandoa hao walikuwa wanagombana kutokana na madai kuwa mwanamke huyo alikuwa anatumia vidonge vya uzazi wa mpango ili asishike mimba jambo lililomkasirisha mwanaume huyo.

Mwenyekiti wa Nyumba Kumi wa eneo lilipotokea tukio hilo Benson Okello ameleeza kuwa baada ya marehemu kuchomwa visu raia wa eneo hilo waliwavamia wanandoa hao na kuwapiga na mpaka sasa wamelazwa ICU kwenye Hospitali kuu ya Pwani ya Mombasa wakiwa mahututi.

“Huu ni uhujumu uchumi, Wote tutawachukulia hatua” –Naibu Waiziri Mwanjelwa

Soma na hizi

Tupia Comments