Michezo

Isikie ofa ya Ashley Young aliyoitoa kwa klabu yake ya Man United..

on

ashleyHuenda hii inatokana na mapenzi yake ndani ya klabu yake ya Manchester United, habari mpya ni kuhusu winga wa klabu hiyo Ashley Young.

Ametoa kauli ambayo pengine ni ngumu kutolewa na mtu yoyote  baada ya kusema yupo radhi kukatwa mshahara wake ili mradi tu aendelee kubaki kuitumikia klabu hiyo msimu mwingine.

Young amekuwa sehemu ya mafanikio ya klabu hiyo baada ya kuonekena kurejesha kiwango chake na huenda akarudishwa katika timu yake ya Taifa lake  England.

Man United ilifanikiwa kuizidi ujanja Liverpool kupata saini ya Young akitokea Aston Villa kwa dau la pauni milioni 17 mwaka 2011 na kumpa mshahara wa pauni 120,000 kwa wiki.

Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza>>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments