Afisa wa serikali nchini Thailand anakabiliwa na shtaka la kuchukua mshahara na marupurupu kwa miaka 10 bila kufanya kazi ipasavyo hata kwa siku moja.
Kesi hiyo kwa mara nyingine imeibua wasiwasi kuhusu ufisadi katika sekta ya umma nchini humo
Kulingana na ripoti, afisa huyo alishika wadhifa katika Idara ya Kuzuia na Kupunguza Maafa katika jimbo la Ang Thong katikati mwa Thailand.
Kulingana na ripoti iliyochapishwa katika gazeti la The Thaiger, afisa huyo alishindwa kupata muda wa kazi yake serikalini kwa takriban miaka 10 kwa sababu ya kujihusisha na kazi ya kuimba kwenye klabu ya usiku.
Afisa huyo alifanya kazi usiku mzima kwenye kilabu kwa sababu hiyo alikuwa anachoka na kukosa kazi ya ofisi wakati wa mchana.
Hata hivyo, mwanamume huyo hakuwahi kufukuzwa kazi au kuadhibiwa kwa utovu wake wa nidhamu na alikuwa akipokea mshahara na marupurupu yake.