Balaza la Halmashauri ya wilaya ya Geita limesema kwa asilimia 95 limetekeleza ilani ya chama cha mapinduzi katika kukamilisha miradi mbalimbali ambayo inaendelea kujengwa na iliyokamilika katika halmashsuri hiyo .
Hayo yameelezwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo , Bi. Khadija Said wakati wa uwasilishaji taarifa ya utekelezaji shughuli za maendeleo ngazi ya kata kwa kipindi cha Octoba na Disemba 2024 huku akikiri kuwepo kwa miradi ya CSR kutokukamilika kwa wakati na kusema miradi hiyo tayari imeanza kutekelezwa.
” Kiukweli tunatekeleza kupitia ilani ya chama cha Mapinduzi katika Halmashauri zetu miradi yote lakini katika miradi tuliyo itekeleza kupitia ilani yetu ya chama cha mapinduzi tuna asilimia 95 kulingana na utekelezaji wa miradi yetu katika Halmashauri yetu , “Makamu Mwenyekiti wa Halmashsuri ya wilaya ya Geita, Khadija Said.
” Katika Halmashauri yetu tuna miradi mbalimbali inayosimamiwa na CSR lakini CSR ni kupitia nguvu za wananchi lakini pia na CSR lakini pia katika Halmashauri yetu tayari tunautaratibu wataalamu wetu wamezunguka kuhakikisha kwamba ile miradi ambayo ina simamiwa na CSR kuangalia kuna miradi mingine tayari inaendelea lakini bado imebakiza hatua ndogo ambayo ikakamilishwe , ” Makamu Mwenyekiti wa Halmashsuri ya wilaya ya Geita, Khadija Said.
Faraji Seif ni Diwani wa kata ya Bukoli amesema katika kata yake wametimiza maagizo ya ilani ya chama cha mapinduzi ambapo mpaka sasa wanaendelea na ujenzi wa jengo la upasuaji pamoja na mradi wa ujenzi wa Maabala unaoendelea huku ujenzi wa zahanati ya Ntono pia ukiendelea.
“Utekelezaji wa Ilani ndani ya kata yangu unaendelea vizuri mpaka sasa hivi tunalo jengo la upasuaji ambalo tunaendelea nalo kwenye finishing lakini pia tunao mradi pale wa maabara unaendelea lakini pia tunayo zahanati ntono inaendelea lakini pia tunayo sekondari mpya ambayo tayari imekwisha anza kwahiyo tumechukua asilimia ndani ya kata yangu ya utekelezaji wa miradi , ” Diwani kata ya ya Bukoli , Faraji Seif.
Nae Diwani wa kata ya Busanda Seleman Gamala amempongeza Mbunge wa Jimbo la Busanda ,Mhandisi Tumaini Magesa kwa kutoa kiasi cha fedha cha zaidi ya shilingi Milioni 22 katika kata hiyo kwa lengo la kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa , Ujenzi wa Daraja pamoja na Ofisi ya kijiji