Askari watatu wa Jeshi la Akiba (Mgambo) ambao Majina yao Bado hayajawekwa hadharani wanaofanya kazi ya kulinda Soko la Wajasiliamari na Ukusanyaji wa Fedha za ujenzi wa Maendeleo katika Kata ya Nyawilimirwa iliyopo wilyani Geita Mkoani humo wanatuhumiwa kwa Makosa ya kuwashambulia wananchi wawili kwa madai ya kushindwa kutoa Mchango.
Hayo yamejiri katika Mkutano wa Mkuu wa Mkoa uliokuwa umeandaliwa kwa ajili ya Kusikiliza kero za wananchi katika Jimbo la Geita ambapo Pendo Michael na Mohamed Rashid wakiwa wahanga wa Matukio hayo wamemweleza Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela mbele ya wananchi juu ya kuwepo kwa Askari hao ambao wameshindwa kufanya kazi yao kwa uadilifu .
“Kuna watu wale Migambo walifika kwangu kudai ela ya Mchango kwamba wanadai ela ya mchango shilingi 7000 nikawambia Mme wangu hayupo haya tupe namba zake za simu nikawapa simu wakaongea naye walipomaliza kuongea naye wakashika baiskeli yangu wapeleke niliwambia Baiskeli nimekodi sio ya kwangu nawaomba mnivumile niende sokoni nikawatafte wa kununua mahindi niwaletee hiyo ela wakakata ndugu Mh Mkuu wa Mkoa nilipigwa sana nilizalilishwa sana , ” Bi. Pendo .
Kwa upande wake Mkuu wa Kituo cha Polisi Nyawilimirwa Inspector. Solomon Lulemkamu athibitisha kuwepo kwa tuhuma hizo huku akikiri kuwakamata na kuwafikisha Mahakamani huku akisema Jeshi la Polisi linaemdelea kushirikiana na Raia wema katika kubaini na kuwakamata waharifu wote katika kata hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela ameiagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa kukaa na kuleta taarifa za Askari hao ikiwemo Majina pamoja na namba zao na kuondolewa kazini na kubaki kuwa raia wa Kawaida ili kufatilia mienendo yao pamoja na Tabia zao.
“Kikao kijacho cha kamati ya usalama cha Mkoa DC unayekaimu hapa nataka mniletee hiyo taarifa cha mwezi unaokuja wa nne niletee ni Askari gani namba gani za uwaskari wamevuliwa wamebaki kuwa raia na tutawafatilia mienendo yao na tabia zao, ” RC. Shigela .