Top Stories

Askari anasakwa kwa kumpa mimba Mwanafunzi

on

Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ulrich Matei amesema bado wanamsaka Askari Polisi wa kituo cha Polisi Kyela Daniel Mlanda kwa tuhuma za kumbaka na kumpa mimba Mwanafunzi wa kidato cha kwanza Wilayani Kyela na kisha kutoroka, Matei amesema wakimpata atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Haikuwa hiari yangu nilikuwa napelekwa na Mama mdogo kwa huyo Askari kwenye eneo lake la Lindo (Benki moja), ananiingiza kwenye chumba kidogo na kuniingilia” – amesema Mtoto huyo mbele ya Kamati inayoratibu siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia” RPC

Licha ya tuhuma za kumpa mimba Mwanafunzi, Askari huyo anadaiwa pia kumzalisha Afisa Mtendaji mmoja na kumtelekeza na Mtoto, pia Mwanafunzi mmoja kutoka Chuo cha Ufundi Kyela anadai kuzalishwa na Askari huyo na kuachwa kwenye mataa licha ya kuahidiwa ndoa hapo awali.

RC MWANRI ATAMANI KUTUMIA HELIKOPTA KWENYE KILIMO “TUTAZALISHA TANI 15,000”

Soma na hizi

Tupia Comments